Mwanablogu Robert Alai atiwa nguvuni na maafisa wa polisi

Mwanablogu mwenye utata Robert Alai ametiwa nguvuni na wanapolisi muda mchache baada ya kuchapisha picha za afisa wa polisi waliofariki katika mitandao ya kijamii.

Soma hadithi hii:

Walinda usalama hawa inadaiwa kuwa waliangamia baada ya kupigwa risasi na wanamgambo wa kundi la Alshabaab katika makabiliano Wajir.

Kamati ya uwiano na utangamano nchini (NCIC) walikuwa awali wametoa onyo kuhusu usambazaji wa picha hizo. Mwanablogu huyu alikuwa amezichapisha katika mtandao wake wa twitter na kufanya picha hizo zisagae mitandaoni.

Kulingana na NCIC , kuchapisha picha za wanapolisi hao kunachangia kulisifia tendo la ugaidi nchini. Hali kadhalika, kunachangia kwa kiasi kikubwa kuwaumiza ndugu, jamaa na marafiki wa maafisa hawa.

Pata uhondo hapa: