Mwanadada aregea nyumbani na watoto 7 baada ya kutoweka miaka 24

agnes
agnes

Kulikuwa na shangwe na nderemo katika kijiji kimoja, kaunti ya Bungoma baada ya mwanadada mmoja kurejea nyumbani baada ya miaka 24, huku akiandamana na na watoto saba.

Mwanadada huyo kwa jina Agnes Nelima alirejea nyumbani kwa mara ya kwanza tangia mwaka wa 1996 ambapo alitoweka na kukimbilia nchi jirani, Uganda pamoja na mumewe.

Kulingana na Bongo 5, baada ya miakahii yote, Agnes alipata kuwa baadhi ua ndugu zake waliaga dunia kufuatia magonjwa huku wengi wakiaga kwa ajili ya uzee.

Kama ilivyo kawaida ya jamii ya wa luhya, tambiko hufanyiwa waliorejea nyumbani baada ya mda mrefu ila Agnes hatofanyiwa kwani ni wanaume pekee hufanyiwa matambiko.

Inasemekana kuwa baadhi ya ndugu zake Agnes walijawa na mshangao mkuu kwani tayari walikuwa wamepoteza matumaini kuwa yuhai au watamuona tena baada ya mda huo wote.