Mwanafunzi mwerevu zaidi wa miaka 9, kufuzu na digrii ya uhandisi

worldlaurent
worldlaurent

Mwanafunzi raia wa Ubelgiji anayesemakana kuwa mwerevu zaidi ulimwenguni, anatarajiwa kufuzu na shahada ya digrii akiwa na umri wa miaka 9 tu.

Laurent Simon kwa sasa anasomea kozi ya uhandisi katika chuo kikuu cha teknolojia cha Eindhoven.

Kulingana na jarida la CNN, Laurent amejitoza kwenye kozi ambayo inachukuliwa kuwa ngumu hata kwa wakufunzi wenye umri wa wastani.

Wahadhiri wake wanamtaja yeye kuwa na ushupavu wa aina yake ikilinganishwa na wanafunzi wengine kote duniani.

Kwa sasa Laurent akiwa na umri wa chini ya miaka 10, anatazamia kuanza masomo yake ya PhD.

Mbali na kuwa mhandisi, Laurent anatazamia kusomea kozi ya udaktari, hili ni jambo linaloajabisha watu wengi sana.

 
Laurent pia ana azma ya kuanza kusomea taaluma ya udaktari baada ya kufuzu na kozi ya uhandisi.
Akihojiwa na kituo cha habari cha CNN, Laurent anasema kuwa anapenda sana kozi ya uhandisi hususan wa elektroniki ila angependa kujua zaidi pia kuhusu utabibu.
Mama yake Laurent anasema kuwa alikula samaki akiwa mjamzito na labda hicho ndicho kilichochangia uweledi wake masomoni.