Mwanafunzi wa chuo kikuu ashtakiwa kwa kumbaka mpenzi wake wa zamani

rapist
rapist
Mwanafunzi wa chuo kikuu alishtakiwa jumatatu kwa kumbaka   mpenzi wake wa zamani  alipokuwa amekwenda kwake kuchukua vitu vyake .

Denis Abuga  alishtakiwa katika mahakama ya kibera mbele ya hakimu mkuu  Abdul Lorot  na alikanusha mashtaka dhidi yake .

Polisi wanasema Abuga  alitekeleza kosa hilo julai tarehe 9  katika kaunti ndogo ya Dagoreti ,Nairobi .

Amedaiwa kufanya ngono na mlalamishi bila idhini yake ,hatua inayochukuliwa kuwa ubakaji . Pia alishtakiwa kwa kosa la pili  kwa kufanya kitendo kisichofaa na mtu mzima kinyume na sheria ya kupambaa na dhulma za kimapenzi .

Mshukiwa alikuwa amempigia simu mlalamishi kwamba angemtembelea ili kwenda kuchukua vitu vyake alivyokuwa ameacha katika nyumba yake .Mlalamishi alikubali .Wakati Abuga  alipofika , mlalamishi alimuacha  sebuleni na kwenda chumba cha kulala lakini Abuga alimfuata na kisha kuketi kitandani .

Ripoti ya polisi inasema  mshukiwa alitaka kuzungumza na mlalamishi  ambaye aliuambia kwamba alikuwa akijitayarisha kwenda anakofanyia kazi . ni wakati huo ambapo Abuga alianza kutumia nguvu na kumshika kisha akamtupa kitandani ,kufunga mikono yake kwa kamba ya mkoba wake na kisha kumbaka .

Aliwapigia simu majirani ambao walimpeleka hospitalini  na kisha baadaye wakaripoti tukio hilo katika kituo cha polisi cha Kilimani .

Hakimu   aliagiza kwamba  mtuhumiwa alipe dhamana ya shilingi laki mbili  na mdhamani wa kiasi kama hicho  na kumuagiza afike katika kituo cha polisi cha Kilimani ili sampuli yake ia DNA ichukuliwe