naomichepkemoi

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Pwani adungwa kisu

Hali tatanishi na wingu la simanzi limegumbika Chuo Kikuu Cha Pwani baada ya tofauti na msukosuko kutokea katika penzi la mwanamme na mpenzi Naomi ambaye ni mwanafunzi chuoni hicho.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, wawili hawa walijipata katika mzozano wakiwa chumbani wanapoishi. Kisirani kati ya mwanafunzi huyu wa mwaka wa tatu kilipelekea yeye kudungwa kisu kutokana na hasira za bwanake

Vurumai na kelele zilipozidi katika chumba hicho ilibidi majirani wawafahamishe polisi ambao walifika kuleta utulivu.

“Maafisa wetu walijulishwa kisa hiki na majirani na kufika pale wakapata bwanake amefunga chumba. Imetulazimu kuvunja na kuingia chumbani kumsaidia bibi yake,” Amesema afisa kamanda wa polisi kaunti ya Kilifi Patrick Okeri.

Naomy walijipata katika majibizano makali na bwanake katika nyumba yao. Inadaiwa kuwa mzozo huu ulianza wakati bwanake alipomtumia Naomi hela za matumizi na kuzirudisha. Kitendo hiki kilimghadhabisha bwanake. Wawili hawa wamebarikiwa na mtoto mmoja.

Afisa kamanda wa polisi kaunti ya kilifi anasema kuwa polisi walisaidia kumuokoa Naomi kutokana na kichapo kikali.

Naomy Chepkomoi amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kilifi akipata matibabu huku bwanake ametiwa nguvuni na maafisa wa polisi kufikishwa kortini jumatatu ili kujibu mashtaka.

Photo Credits: facebook

Read More:

Comments

comments