Mwanafunzi wa kidato cha kwanza azuiliwa kwa mauwaji

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika kaunti ya Homa Bay anazuiliwa kwa tuhuma za mauwaji baada ya kudaiwa kuwa alimwangamiza msichana wa miaka 11 eneo la Rachuonyo.

Mshukiwa huyo anadaiwa kutekeleza uovu huo katika kijiji cha Nduga ,lokesheni ya Kachien kaskazini.

Mwili wa msichana huyo ulipatikana kama umefichwa kwenye shamba la mahindi.

Baada ya upasuaji kufanyika ,ilibainika kuwa mwendazake alifariki kutokana na kugongwa kwa kifa butu ubafuni.

Kamishna wa polis Esau Ochorokodi amedhibitisha kutiwa mbaroni kwa kichana huyo wa miaka 15 na kuzuiliwa katika kituo cha polis cha Kasele akisubiri kufikishwa mahakamani.