Mwanahabari wa K24 afariki dunia akiwa safarini kumwona mkewe aliyejifungua

WhatsApp Image 2019-11-21 at 12.55.52 (1)
WhatsApp Image 2019-11-21 at 12.55.52 (1)
Mwanahabari  amefariki dunia baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani katika mto wa Kerio .

Daniel Chemjor ambaye ndiye mwendesha vipindi vya televisheni ya K24, aliaga dunia gari lake lilipotumbukia katika mto Kerio kwenye barabara ya Iten - Kabarnet.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa Jumatano ambapo anasemekana alikuwa safarini kumwona mkewe aliyekuwa amejifungua.

Gari aina ya Toyota Premio iliopolewa kwenye mto huo ndani yake kukiwa na mwili wa Chemjor.

Polisi wamethibitisha kisa hicho na kukiri kuwa mwili huo ni wa mwanahabari Daniel Chemjor.

Gari hilo lilianguka kutoka mwinuko wa Cheploch yenye umbali ya zaidi ya mita 200.

Maarufu kama Cheploch George, ni mpaka baina ya kaunti ya Baringo na Elgeiyo Marakwet.

Aidha, inasemekana gari hilo lilipoteza mwelekeo  barabarani na kutumbukia mto huo.