Mwanahabari mwenye asili ya kiafrika ashikwa na polisi katika maandamano yanayoendelea Amerika

unnamed (8)
unnamed (8)
Maafisa wa polisi katika mji wa Minnesota Amerika wamemtia ndani mwanahabari wa shirika la CNN mwenye asili ya Kiafrika Ijumaa akiripoti kuhusiana na maandamano yanayoendelea katika jimbo hilo baada ya kuuwawa kwa George Floyd na polisi fedhuli asiye na utu.

Katika video hiyo inayosambaa mitandaoni kwa sasa,maafisa hao wanaonekana wakimzunguka mwanahabari Omar Jimenez kabla ya kumtia pingu.

Omar anasikika akiwataka maafisa hao kumwachilia kufanya kazi japo wito wake unaambulia patupu .

"This is the four of us. We are one team. Put us back where you want us. We are getting out of your way," Omar aliwambia polisi.

Kikosi hicho cha CNN kilikuwa kinafanya taarifa kuhusiana na waandamanaji waliokuwa wanaandamana kuhusiana na hatua ya kuuwawa kwa Floyd mapema wiki hili.

Rais wa Amerika Donald Trump amekashifu maandamano hayo akisema hatakubali kisa hicho kuendelea kamwe.

Mauwaji ya Floyd wamekashifiwa vikali na Jumuiya ya Afrika chini ya uongozi wake Moussa Faki Mahamat .

Faki amesema bara la Afrika linakashifu vikali ubaguzi wa rangi unaonezwa na baadhi ya viongozi wa Amerika.

Aidha ujumbe ambao Trump alikuwa ametuma kwa mtandao wake wa Twitter uliondolewa na wakuu wa mtandao huo kwa kile walisema ni kueneza vita dhidi ya binadamu.