Mwanahabari Rashid Abdalla aomboleza kifo cha muigizaji Pretty Mutave

Mwanahabari wa runinga ya Citizen Rashid Abdalla anaomboleza kifo cha muigizaji Pretty Mutave, kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram Rashid alimsifu muigizaji huyo kwa kipaji cha uigizaji.

Huku akiposti picha yake Rashid aliandika ujumbe ufuatao,

“ Japo kazi ya Mungu haina makosa lakini msiba hauna mazoea. kipaji chako kikawe nuru kwa malaika. Mola ailaze roho yako pema peponi Inshallah. Heshima na kipaji chako vitadumu milele”. Aliandika Rashid.

https://www.instagram.com/p/CFJShohDWrO/

Kifo cha Muigizajii huyo hakijabainika, alikuwa kwenye mitandao ya kijamii huku akiacha kuonekana kwenye mitandao hiyo mwishoni mwa mwezi jana.

Mutave alifahamika sana kupitia kwa kipindi cha Maza kilichokuwa kinapeperushwa kwenye runinga ya Maisha Magic East, na pia kwenye kipindi cha Aziza ambapo Rashid Abdalla na mkewe Lulu Hassan ndio wazalishaji wa vipindi hivyo.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.