Ndoa ya Sekunde; Mwanahabari wa runinga ya Inooro asimulia jinsi ndoa yake ilivunjika

Winnierose-mpasho-696x464
Winnierose-mpasho-696x464
Mwanahabari wa runinga ya Inoora na mwanamuziki wa nyimbo za Injili Winnie Rose Wangui alisimulia jinsi ndoa yake ilivunjika nakujutia ni kwa nini alifunga pingu za maisha kwa njia ya harusi.

Akizungumza katika mahojiano katika mtandao wa kijamii wa youtube Winnie alisema.

"Tulienda katika njia tofauti, na fikiri alipata mke mzuri kuniliko, na maisha yaliendelea." Alisema Winnie.

Winnie aliulizwa nini kilichosababisha yeye na mume wake kutengana, alisema kuwa hamna haja ya kuhukumu na wakati walikuwa wanapanga harusi yao hakukuwa na makubaliano kati yao.

"Tulijaribu kusuluhisha mambo yote lakini si kwa amani, kilicho fuatia ni tutaelewana.kwa sasa yuko na familia ambayo mimi sina." Alisema Winnie.

Alisema sasa  anaeza tabasamu kwa sababu halikuwa jambo rahisi kamwe na hakudhani lingeweza tokea .

"Tulitengana nikiwa na mimba, kwa hivyo nilikaa miezi tisa pekeyangu, na ilibidi nianze maisha tena, kutoka kununua kijiko, lakini safari ya uja uzito wangu ulikuwa na changamoto nyingi kwa maana kuna uvumi na maneno mengi ambayo yalikuwa yanazungumzwa

Nilijitenga na watu wote hata marafiki zangu na kubaki na marafiki wachache." Alisema.

Alisema kilichopelekea wawili hao kutalakiana ni kutokana na mawasiliano mabaya baina yao yaliyopelekea uhusiano wao kuharibika .

Alipokuwa anajifungua Winnie alitia saini mkataba wa daktari kwa maana alikuwa anaenda kufanyiwa upasuaji ili ajifungue.

"Nilichokuwa nataka ni amani na kumshika mtoto wangu,nilikuwa katika wadi ya kibinafsi, kwa maana sikuwa nataka mtu katika wadi yangu." Winnie Alizungumza.

Aliongeza kuwa japo anamlea mwanawe pekee yake hatawai jutia kamwe na hata hatawai amini mtu yeyote katika maisha yake.

"Nilipoenda katika chumba cha upasuaji nilikuwa pekeyangu na nambari ya simu niliopeana ilikuwa ya mama yangu ambaye nilimpigia simu baada ya upasuaji." Aliongea.

Mwanahabari huyo alisema hajui muda ambao mume wake alichukuwa ili aoe tena lakini anachojua nikuwa mtoto wake yupo karibu kutoshana miaka na mwanawe.

Aliwaimiza watu waweze kungoja wakati wa Mola kwa maana ndio wakati bora .