Mwanamke afariki baada ya kupatikana chumba kimoja cha kulala Mtito Andei

Kifo
Kifo
Mwanamke 25, afia daguroni Mtito Andei.

Maafisa wa polisi huko Mtito Andei kaunti ya Makueni wameanzisha uchunguzi baada ya mwanamke mwenye umri wa miaka 25 kupatikana amefariki kwenye chumba kimoja cha kulala mjini humo.

Kulingana na naibu OCPD wa Kibwezi Geoffrey Nderitu, mwili wa mwendazake ulipatikana na wafanyikazi wa eneo hilo la burudani walipokuwa wakifanya usafi.

Nderitu anasema bado haijabainika iwapo mwanamke huyo alikuwa na mpenziwe alipokodi chumba katika eneo hilo linalotumiwa sana wafanyibiashara wa ngono.

Mwili wake umehifadhiwa katika hifadhi ya  maiti ya Makindu huku uchunguzi ukianza.

-Solomon Muingi.