Mwanamke akamatwa kwa madai ya kushiriki mapenzi na mvulana wa sekondari

gang
gang
Mwanamke alikamatwa katika mji wa Ndhiwa Jumapili asubuhi kwa madai ya kushiriki mapenzi na mvulana wa kidato cha tatu.

Wanakijiji wanasema kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 25, alimrai mvulana huyo kushiriki mapenzi naye ili ampe pesa.

Mwanamke huyo anasemekana kuwa mhasibu katika baa moja na amekuwa akishiriki mapenzi na kijana huyo  barobaro tangu shule ilipofungwa Oktoba.

 Mnamo Jumamosi, babake kijana huyo aligundua kuwa mwanawe mwenye umri wa miaka 17 amepotea kwa siku nne mfululizo.
 Mkufunzi aliyekuwa ameajiriwa kumpa mafunzo ya ziada kwao alilalamika kuwa mvulana huyo huwa nadra kuonekana.
Babake anasema kuwa alienda na polisi katika nyumba hiyo na kumpata mwanamke akilala naye.
ALitiwa mbaroni na kushtakiwa katika kituo cha polisi cha Ndhiwa.
Wanakijiji wakiongozwa na Bernard Ogallo alionyesha kufadhaishwa na tabia za mwanamke huyo.

Mkuu wa polisi katika Ndhiwa Evans Ombui alisema kuwa uchunguzi utafanya ili kubaini iwapo mwanamke huyo alimbaka mvulana huyo barobaro na kufikishwa mahakamani Jumatatu ili kijibu mashtaka ya ubakaji.