Mwanamke akiri kumchoma mwanawe kwa kuiba sadaka

agnes mutua
agnes mutua
Siku ya Ijumaa, mwanamke mmoja alikiri kortini kuwa alitumia karatasi moto kuchoma kichwa, tumbo na viungo vingine vya mwili vya mwanawe.

Agnes Mutua alikubali mashtaka hayo mbele ya mwanasheria mkuu wa mwandamizi wa Kibera, Esther Boke akisema alikasirishwa na mwanawe baada ya kuiba fedha ambazio alinuia kutoa kama sadaka.

Mutua alimshambulia mwanawe Stephen Kalonzo Musyoka mnamo July 14 Kibera, Bombolulu Nairobi.

Inakisiwa Musyoka alichukua zile fedha wakati mamake alikuwa anaomba wakati wa huduma ilikuwa inaendelea na akaamua kununua mandazi na zile fedha.

Alikamatwa baada ya msamaria mwema kumuona mtoto yule na majeraha akielekea nyumbani kutoka shuleni na baada ya kumuuliza maswali, ndipo kijana yule alipo fichua kilichotendeka.

Msamaria huyo mwema alimpeleka kijana huyo kliniki ya kibinafsi alipo tibiwa kabla ya mshukiwa kukamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kilimani.

Mutua alijitetea akisema kuwa shetani ndiye alimuingia na kuamua kumuumiza mwanawe huku akisema hakuwa anajua alichokuwa akifanya.

Hakimu huyo aliamuru ripoti kuhusu kesi hiyo iandaliwe kabla ya siku ya kuhukumiwa kwake Mutua, Julai 28.