Sophia aliye wapiga polisi filamu waki mnyanyasa mwanamke hatashtakiwa

sophia Njeri
sophia Njeri
Mwanamke aliye kamatwa kwa kuwapiga polisi wa trafiki filamu wakimnyanyasa abiria wa mwanamke Nairobi jumanne hatashtakiwa.

Hii ni baada ya ofisi ya DPP katika mahakama ya Makadara kukataa mashtaka dhidi yake, mashtaka yalisema kuwa mwanamke huyo hakuwa na nia ya uhalifu.

"Hatuwezi mshtaki mtu kwa sababu polisi wamemshika kwa kuwachukua filamu wakifanya kazi yao, tulikataa faili hiyo kwa sababu si uhalifu kuchukua filamu katika umma,"Alieleza mmoja wa mwendesha mashtaka.

Walisema kuwa polisi wanapaswa kuwa  na ushaidi tosha ili kumshtaki mshukiwa."Hatutaki kuchukua kesi ambazo hazina ushahidi wa kutosha ama kesi ambazo mahakama itaenda kukataa,"aliongezea.

Alisema kuwa DPP Noordin Haji alikuwa ameitisha faili ya kesi hiyo.

Sophia Njeri alishikwa kisha baadaye akaachiliwa na dhamana ya shillingi 10,000 alikuwa aende mahakamani leo ili kupokea mashtaka, katika filamu hiyo Njeri alionekana akiwachukua polisi wakimvuruta mwanamke kutoka kwa kiti ya matatu katika eneo la Kasarani barabara ya Nairobi CBD.

Jumanne polisi wa kusimamia mamlaka na kujitegemea (Independent Policing Oversight Authority) wakifanya hatia kwa kumkamata Sophia.

Walisema kuwa walikuwa wamepeleka jambo hilo katika kituo cha polisi cha Kasarani, katika filamu hyyo polisi 5 walionekana wakijaribu kumtoa mwanamke katika matatu moja.

Mwanamke huyo hakuweza kubali awe mnyonge aliweza kujitetea na kuuliza sababu zake za kutolewa katika kiti cha mbele katika gari hiyo,

Sophia pia hakulaza damu alipoona kitendo hicho aliweza pia kumtetea mwanamke huyo na kisha kuchukua filamu hiyo ambayo ilimueka mashakani.

Polisi hao walipoona kuwa Sophia ana rekodi waliweza kumtishia ilhali hakuweza kutishika bali aliendelea kurekodi kisa hicho.

Ni siku Sophia atakayo kumbuka katika akilini mwake kwa kutoshtakiwa na kuachiliwa huru licha ya kutoka na dhamana ya shillingi 10,000.