Mwanamke aliyekamatwa na karatasi bandia kufikishwa kortini

Mwanamke ambaye alipatikana na karatasi bandia ya ushuru katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta akitoka nchini China, anatarajiwa hii leo kufikishwa mahakami kujibu mashataka hayo.

Jane Mary Muthoni Gichengo anatuhumiwa kuwa mmoja wa watu wanaofanya makosa ya jinai mtandaoni ambao hufanya mihuri ya ushuru nchini China na kuhamisha Kenya.
Mamlaka ya mapato nchini Kenya (KRA), imesema mihuri hiyo zinasafirishwa kupitia gari la shirika hilo mpaka kwa kampuni ya kutengeneza na kusambaza pombe, jambo ambalo linachangia watu ama pia kampuni kutolipa ushuru kwa serikali.

 KRA ilitangaza kuwa wamepoteza karibu shilingi billioni moja kutokana na mikataba hayo ambayo si halali.