Mwanamke amtema mumewe na wanawe baada ya kupoteza kazi wakati huu wa corona

Ni mambo ambayo  wanandoa wengi wanazidi kushuhudia hasa wakati huu wa janga la corona huku wengi wao wakiachwa wakiwa na upekwe na kusongwa na mawazo chungu nzima.

Mwanamume mmoja kutoka eneo la Rongai alisongwa na mawazo baada ya kuachwa na mke wake na kukusanya virago vyake kisha kumuachia wanawe.

Lakini sababu ni ipi? Kilonzo alipoteza kazi wakati virusi vya corona viliporipotiwa humu nchini, wengi walipoteza kazi zao huku wakitorokwa na wake zao au waume wao.

Kilonzo alisema kuwa mkewe alianza na kutompa heshima na hata kuanzisha matusi kila mara,

"Lilikuwa jambo la aibu nilijaribu mara nyingi kuzungumza naye bali hakusikia, alikusanya virago vyake na kisha kuondoka na kila kitu chake

Aliniachia wanangu nilijaribu kumbembeleza lakini nguvu zangu ziliambulia patupu kwa maana aliniambia kuwa siwezi nikatimiza mahitaji yake licha ya vile haki hiko humu nchini

Nimekuwa nikifiria sikuwa natimiza mahitaji yake muda huo wote." Alieleza Kilonzo.

Nguvu zake za kumtafuta na hata kumpigia simu ili ajue hali yake hazilifua dafu kwa maana mkewe hakupokea simu zake.

Kilonzo ana hofu ya kutowalea wanawe iwezavyo licha ya uchumi kuwa mgumu hasa wakati huu nchi inakabiliwa na janga la virusi vya corona.