Mwanamke amuua mumewe kwa kumdunga kisu Eldoret

kisu
kisu
Polisi mjini Eldoret wamemkamata mwanamke aliyemdunga mumewe kwa kisu na kumuua jana usiku katika mtaa wa Shauri Estate, mjini Eldoret.

Marehemu alikuwa dereva wa teksi na alifika nyumbani usiku wa manane alipotoka kazini, baadaye wawili hao walianza ugomvi kuhusu ujumbe aliopokea na hapo vita vikaibuka dhidi yao wawili.

Jirani yao, bi Pauline Kibe alisema kuwa waliskia ugomvi na mayowe ndani kutoka kwa nyumba hiyo lakini juhudi za kumuokoa jamaa huyo hazikufua dafu kwani alifariki papo hapo baada ya kudungwa kisu kifuani.

Polisi waliofika eneo hilo la tukio walianzisha uchunguzi na wakaupeleka mwili katika chumba cha kuhifadhia mauti cha hospitali ya Moi.

Hayo yakijiri,

Wizara ya afya katika kaunti ya Taita Taveta itawapa ajira za kudumu zaidi ya wahudumu wa afya 200 wanaohudumu kwa kandarasi ili kukabili changamoto ya uhaba wa wahudumu. 

Waziri wa afya kaunti hiyo Daniel Makoko anasema huduma ya afya ina upungufu wa wahudumu 400 huku akilitaja swala hilo kama changamoto kubwa katika kutoa huduma kwa wakazi.

Anasema wahudumu wengi wa afya wanashawishika kuhamia kaunti zinazotokana ajira ya kudumu na jivyo kusababisha uhaba katika kaunti hiyo.