Mwanamke kulipa Sh250,000 baada ya kufichua hali ya wenyewe ya Ukimwi

Mwanamke aliyefichua hali ya mwenzake ya Ukimwi wakati wa mzozano ameagizwa na tume ya HIV kulipa Sh250,000.

Mahakama iliamuru kwamba mhojiwa alikuwa amekiuka vifungu vya sheria vya HIV and Aids Prevention and Control Act wakati alipofichua hali ya mwenzake kuwa ana virusi vya HIV.

Korti ilisema vitendo vya mhojiwa ni vibaya na sio halali na maelezo hayo hayakufaa.

Mshtakiwa SNW alikuwa ameshtaki A.G. kwa kufichua hali yake ya Ukimwi wakati alikuwa na mgeni. Isitoshe, mwanawe pia alikuwepo.

Kulingana na waraka wa korti, SNW alikuwa akiishi na A.G. nyumbani kwake huko Parklands, Nairobi, wakati walipokosana.
Mshtakiwa alisema kwamba mnamo Februari 17, 2018, mhojiwa alirudi nyumbani kwao lakini akakataa kuingia.
“SHE STOOD AT THE DOOR AND DEMANDED THAT I BRING HER CLOTHES AND OTHER PERSONAL ITEMS. I, HOWEVER, DECLINED TO DO SO,” SNW ALISEMA.

Alisema ni wakati huo ndipo A.G. alipoanza kumtukana mbele ya mtoto wake na rafiki yake ambaye alikuwa akimfariji kufuatia kifo cha baba yake.

“A.G. CLAIMED I WAS GOING TO DIE SINCE I WAS HIV POSITIVE. I WAS SHOCKED HOW SHE FOUND OUT ABOUT MY STATUS YET I HAD NOT DISCLOSED THAT INFORMATION TO HER,” ALISEMA.

Mshtakiwa baadaye aligundua rafikiye alijua kuhusu hali yake kutoka kwa jirani ambaye nyumba yake alihamia baada ya kuondoka.

Hapo awali, jirani alikuwa amemtusi na pia kufichua hali yake.
Shahidi aliyetambuliwa kama RW alisimama mbele ya mahakama na kutoa ushahidi dhidi ya mhojiwa.
-The Star