Crime scene

Mwanamme mmoja apatikana ameaga kwenye kambi la polisi huko Busia

Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 20 amepatikana ameaga dunia kwenye chumba kimoja katika kambi la polisi wa utawala ya Malambisia eneo bunge la Butula kaunti ya Busia kwa njia ya kutatanisha.

Inadaiwa mwanaume huyo alikamatwa na maafisa wa polisi wakati wa usiku kwa tuhuma za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana mmoja katika eneo hilo, na wananchi wanadai alipigwa na maafisa hao kabla ya kufunga nguo shingoni na kudai kuwa alijitia kitanzi.

Kwingineko

Kinara wa ANC musalia Mudavadi amewataka wakenya kuunga mkono usajili wa huduma namba akisema hatua ya viongozi wa upinzani kuunga mkono zoezi hili ina maana kuwa sio swala la serikali bali ni la manufaa kwa wakenya

Akiongea mjini Kakamega, Mudavadi amesema usajili wa huduma namba utahakikisha kila eneo linapata mgao sawa kulingana na idadi.

Kwingineko

Washika dau katika sekta ya mazingira wameelezea wasi wasi wa kaunti ya Taita Taveta kuendela kukabiliwa na changamoto za mabadiliko ya hali ya anga kufuatia hatua ya kuendelea kuchomwa kwa misitu mikuu eneo hilo, kukatwa miti kiholela na uharibifu wa chemchemi za maji.

Mwanamazingira Esther Mwanyumba anasema kwa mda wa juma moja sasa misitu kadha imechomwa, hali ambayo anasema iwapo haitathibitiw, huenda eneo hilo likakuwa jangwa hivi karibuni.

Ameitaka jamii ya Taita Taveta kutupilia mbali dhana potofu kuwa uchomaji misitu kunavutia Mvua.

Click here for more

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments