water

Mwanamume Bungoma aoshwa kwa kutoa uvundo

Mwanaume wa miaka 28 aliogeshwa kwa lazima na wakaazi wa kijiji cha sasuri katika eneo bunge la Kanduyi katika kaunti ya Bungoma baada ya kusemekana kuwa amekuwa akiishi bila kuoga kwa muda.
Wakaazi wa kijiji hicho wakiongozwa na mwenyekiti wa ukoo wa Basimaolya John Sitati anasema hawakupendezwa na uvundo aliokuwa nao mwanaume huyo haswa walipokuwa wakinywa pombe katika kituo kimoja katika kijiji hicho.

Iliwabidi wakaazi wa kijiji hicho kumfuata mbio alipokuwa akihepa kutoka katika kituo cha pombe walipokuwa wakinywa na kujificha chooni jambo lililopelekea wakaazi hao kumtoa chooni kimabavu na kumuosha.
Sitati amedai kuwa wananuia kuendelea kufanya hivyo kwa kila mtu wa ukoo huo anaye hepa maji hadi wawe safi.

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments