Mwanamuziki Pitson afichua kilichomfanya apotelee mziki kwa mda

Mwanamziki Pitson Ngethe Githinji almaarufu Pitson akizungumza na RadioJambo katika kipindi cha bustani la Massawe alifichua kuwa amerudi tena kuwaburudisha mashabiki wake, baada ya mapumziko ya mda unaozidi mwaka mmoja.
"Nimepotea kwa sababu ya mambo kadhaa kwanza kuwa mzazi wa watoto wawili, pili nilizingatia uandishi sana ambapo nilikuwa naandikia wanamuziki wengine nyimbo za injili na ushirika.

la tatu mimi ni kiongozi wa nyimbo za ibada katika kanisa la Karura chapel ambapo nilikuwa nachukua muda wangu wote, lakini sasa nimerudi, wasanii wa kenya wa nyimbo za injili tunapaswa kuamka na kutoa maudhui,"Alisema pitson.

Akizungumzia ndoa yake, Pitson alimjua mkewe mwaka wa 2006 na kisha kumuoa mwaka wa 2013 ambapo wamebarikiwa na watoto wawili. Kifungua mimba ana miaka 3 huku wa pili akiwa na mwaka mmoja.

Msanii huyo alijiandikia wimbo Niache niimbe na kisha kwenda mapumzikoni, lakini amerudi na wimbo ambao amemhusisha Amani G msichana wa miaka 13 kutoka Githurai.

"Amani G ni msichana wa miaka kumi na tatu kutoka Githurai ambaye amekuwa msaani mkubwa alielekezwa kwangu na pinecreek niliitwa kumwandikia nyimbo nampenda Amani G kwa sababu anapenda kazi yake." Pitson aliongezea.

Mwanamzuki Pitson alikuwa masomoni sana alipokuwa mapumziko lakini sasa amerudi ili kuendeleza talanta yake ya muziki kwa maana hakusomea uanamuziki lakini ni talanta ambayo amekuwa nayo tangu utotoni.

Alianza muziki akiwa katika shule ya upili ya Eastliegh.

Alijiunga na chuo kikuu cha JKUAT ambapo alikuwa anasomea B.COM.

Pitson aliandika nyimbo 50 kabla wimbo wake wa kwanza Lingala ya yesu, kuchezwa kwa mara ya kwanza DJ Croba.

Skiza uhondo wote.