Mwanangu yuko kwenye kwarantini, waziri Kagwe afichua

unnamed (4)
unnamed (4)
Waziri Mutahi Kagwe alifichua kuwa mwanawe wa kiume  pamoja na mpwa wake wako kwenye kwarantini.

"This is not a forced quarantine but a mandatory exercise as advised by the government. You are not being quarantined because  you have committed a crime but to keep you safe. All you need to do is cooperate with the health and security officials,” alisema.

“I have a son and a niece who is in quarantine and there is no offense in taking preventive measures”.

Kagwe alisema alipimwa ila hakupatikana na COVID-19.

Kagwe alisema kuwa watu wote waliotangamana na wagonjwa wa Covid-19 watalazimishwa kuwekwa kwenye kwarantini.

Kagwe alisema watu hawa watachukuliwa na kupelekwa katika vituo vya kwarantini.

Aliwaomba watakaochukuliwa kuwajibika.

Vilevile Kuna visa 7 vipya vya COVID-19.

Visa vyote vimeripotiwa kutoka kaunti ya Nairobi huku vikifikia 28 sasa.

Saba hao, wanne ni wakenya, 2 kutoka Congo na mchina mmoja.

Visa vya watu waliopatikana na virusi hivyo sasa vimefikia visa 38.

Wanne kati yao wamekuwa wakisafiri mara kwa mara, mmoja alisafiri kutoka Mombasa.

Wawili wakiambukizwa baada ya kutangamana na watu walio na virusi hivyo.

Hata hivyo, mgonjwa wa kwanza na wa tatu wamepona kufikia sasa.

Uchunguzi wa pili utafanywa baada ya masaa 48 kutoka sasa.

Siku ya Ijumaa Mutahi alisema kuwa Nairobi ndio inayoongoza na visa vya COVID-19 huku ikiwa na wagonjwa 29.

Kaunti zingine zilizoathirika ni pamoja na kilifi (6) Mombasa (2) Kwale (1) na kajiado (1)