Mwanasiasa atuma ujumbe wa mapenzi kimakosa kwenye kundi la Whatsapp

Mwanasiasa maarufu sana nchini alijipata katika hali ya fedheha machoni pa wananchi wake.

Kiongozi huyo alituma ujumbe ambao ulinuiwa kwenda kwa kidosho mpenziwe wa kando kwenye kundi la Whatsapp.

Hata ingawa alifaulu kufuta ujumbe huo kundini, lakini tayari wanachama kwenye kundi hilo walikuwa tayari washaisoma kwa mshangao mkubwa.

Moja wao aliambia makala ya upekuzi kwamba mbunge huyo wa zamani alikuwa anamwuliza kidosho jinsi alivyofurahia safari yao pamoja kwenye gari la Range Rover Sports.

Makala ya upekuzi yalibaini kuwa kidosho huyo ni msanii wa Afrika mashariki.

Mwanamuziki huyo anasemekana kuibadilisha rangi ya gari alilopewa baada ya kupokonywa kutoka kidosho mwingine.