Mwanaume aliyetuhumiwa kumuua mkewe alikuwa amemakinika kanisani

Mwanaume ambaye yumo mikononi mwa polisi kwa madai kuwa alimuua mkewe alikuwa mchangamfu katika miradi ya kanisani.

Pia aliweza kuwasaidia wasiokuwa na uwezo, rafiki yake wa kutoka utotoni alisema.

Katika ujenzi wa kanisa la AIPCA Kimatongu katika eneo la Mweiga kijiji cha Kieni west aliweza kusaidia katika ujenzi huo.

Joseph Karue, 41, na mpenzi wake Judy Mungai wametuhumiwa kwa kumuua Mary Wambui, 39.

Wambui mama wa watoto wawili alitoweka Januari 26 na kisha mwili wake kupatikana katika maeneo ya Juja katika mkahawa wa Courtesy beach.

Mnamo Jumanne wawili hao walipelekwa mahakamani mbele ya hakimu mkuu Stella Atambo na wala hakuchukua ulalamishi wowote na kuwapa wachunguzi siku 14 ili waweze kuchunguza kisa hicho

Polisi jana waliweza kupata gari ya aina ya Mercedes Benz ya mwendazake Wambui karibu na eneo la Juja na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Ngewa kijiji cha kwamaiko kata ngogo ya Githunguri.

Rafiki wa utotoni wa Joseph alimjua kama Mwangi Karue, alipatwa na butwaa walipo ona picha ya mshukiwa Karue katika mitandao ya kijamii kuhusiana na mauaji hayo.

"Huwa ana hudhuria maendeleo mengi ya kanisani pia ni yeye amesaidia pakubwa katika ujenzi wa kanisa la AIPCA Kimatongu na alihudhuria harambee kadhaa."mkazi mmoja alisema.

Ni wangapi ambao wamejificha kanisani ambao wanasema kuwa wao ni wazuri ilhali na kinaya cha maneno na matendo yao?

Walio kuwa wanafunzi wa zamani katika shule ya msingi ya Kairuthi wadi ya Iria ,Othaya, Nyeri walisema kuwa Karue alifanya mtihani wake wa msingi katika enzi za 1990s na hakuwa ata mwerevu.

Waliongezea na kusema ni maajabu vile aliweza kufaulu kimaisha na mali nyingi, ingawa alizaliwa Othaya familia yake ilihama wakaenda Mweiga eneo la kieni 1990s.

Baba yake alikuwa afisa wa elimu na mama yake alikuwa mfanyikazi katika benki (bank teller).

George aliandika katika mtandao wake wa kijamii (Facebook) kuwa Karue alikuwa mwanafunzi katika shule ya upili ya Kenyatta High, Mahiga darasa la 1999.

Mkazi mmoja pia Joseph aliweza kujiunga na sekta ya matatu kutoka barabara ya Jogoo-Buruburu kisha Nairobi.

Pia aliongezea na kusema kuwa Karue alikuwa anasambaza miti ya umeme kwa hivyo kazi hizi zinaweza changia katika utajiri wake.

Kulingana na ripoti mpenzi wake alikuwa anaishi katika nyumba ya kukondisha ya ksh60,000 kwa mwezi.

"Hakuna mtu katika familia yao ana mali kama Karue,"Alisema rafiki mwingine.

Karue hakuwa anasema mambo yake au tatizo lake kwa mtu asiye mjua vizuri, miaka saba au nane iliyopita Karue aliweza kuwaitia marafiki zake sherehe ambayo wanasema kulikuwa na nyama na pombe kwa wingi.

Pesa, biashara na mali alitoa wapi kama hakuwa mwerevu darasani na kwanini asiseme utajiri wake ulitoka wapi ni maswali ambayo watu, familia na marafiki wanajiuliza na watazidi kujiuliza.