Mwanaume amuua mkewe wa wiki tatu kwa kumdunga kisu

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 25 ametorokea mafichoni baada ya kumuua mkewe kwa kumdunga visu katika kijiji cha Khujibi eneo bunge la Matayos kaunti ya Busia.

Wanakijiji wakiongozwa na mzee wa kijiji hicho Luka Ochieno manande wanasema mwanaume huyo alianza kumpiga mkewe wakati wa usiku kabla ya wao kuingilia kati ingawa mkewe alifariki baadaye kutokana na majeraha ya visu.

Wanadai kuwa wawili hao walikuwa wameoana kwa muda usio zidi majuma matatu kabla ya mwanaume huyo alie na mke mwingine kutekeleza unyama huo.

Kwingineko katika kijiji cha Bukalama eneo hilo hilo la Matayos, mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 55 anaendelea kupata nafuu baada ya kuumwa sehemu zake za siri na mkewe.

Mwanaume huyo ameongeza kuwa mbali na mkewe kmujeruhi, pia alitoweka na mali yake ikiwemo mifugo, na sasa anaomba asaidiwe kisheria na kimatibabu.

-Leonard Acharry