Mwanaume apigwa risasi na kufariki akijarjibu kumpokonya polisi bunduki

police with gun
police with gun
Mwanaume amepigwa risasi na kufariki papo hapo baada ya jaribio la kumpokonya bunduki afisa wa polisi kutibuka, Alhamisi.

Jamaa huyo ambaye hakutambuliwa haraka anasemakana kujaribu kumpokonya bunduki afisa wa polisi aliyekuwa anashika doria katika benki ya Gulf Mombasa.

"Iwapo angejua jinsi ya kufyatua risasi watu wengi wangeuliwa, " Dan Mutembei ambaye alishuhudia alisimulia.

Mutembei anasema kwamba afisa mwingine wa polisi aliingilia kati na kumuua jamaa huyo.

Mwili wake umepelekwa katika hospitali ya Coast General.

Visa kama hivyo vya raia kuwapokonya risasi maafisa wa polisi vimekithiri katika eneo la Bondeni tangu mwaka wa 2012-2016.

Hata hivyo, kuna madai kuwa jamaa huyo ana akili punguani.