Mwanaume ashikwa kwa kumbaka mama mzazi

Mwanaume mmoja atarajiwa kuenda mbele ya mahakama baada ya kudaiwa kumbaka mama mzazi.

Mama huyu alikuwa akielekea nyumbani pekee yake baada ya kutoka kwenye baa.

Mshukiwa huyu alikamatwa Jumamosi baada ya mama yake ambaye ana umri wa miaka hamsini kumtambulisha kama mshukiwa wa tendo hilo katili.

Ripoti zashauri kuwa mwanaume huyo ana umri kati ya ishirini na nane na ishirini na tisa.

Kituo cha habari cha News 24, ilisema kuwa mama huyo alikuwa anatembea kwenye mtaa aliposkia nyayo nyuma yake kabla ya kushambuliwa.

Msemaji wa askari alisema;

''Inadaiwa kuwa mwathirika alikuwa anatembea kutoka kwa baa ya mtaani wakati wa saa moja. Alikuwa anaelekea nyumbani. Mwathirika aliskia nyayo nyuma yake. Aliendelea kutembea hadi mtu aliyekuwa nyuma yake alipomnyakua. Alikokotwa mbali na barabara na mshukiwa akamvamia. Mshukiwa kisha alimbaka.''

Mshtakiwa alitoroka eneo hilo la uhalifu kabla ya mama yake kumtambulisha kwa polisi kama mtoto wake wa uzazi.

Mwanaume huyu ameshtakiwa kwa ubakaji.