Mwanaume ashtakiwa kwa kuuma sehemu nyeti za mwanawe

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 23 huko Voi, kaunti ya Taita Taveta amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumuuma na kumkata uume wake mwanawe mwenye umri wa miezi minne.

Salim Chongo anadaiwa kutekeleza kitendo hicho Cha kinyama nyumbani kwake mtaa wa Mwingoni mnamo Octoba 13 mwaka huu.
Ameyakana mashtaka hayo mbele ya hakimu mkaazi Fredrick Nyakundi na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu ishirini. Kesi hiyo itasikizwa Oktoba 31.

Hayo yakijiri, wananchi kutoka eneo la Changara kaunti ndogo ya Teso kaskazini kaunti ya Busia wamejitokeza kulalamikia kusitishwa kwa mradi wa ujenzi wa bwawa eneo hilo wa kima cha shilingi milioni 24.

Wananchi hao wamelalamikia hatua ya mwanaharakati mmoja ya kuiandikia benki ya dunia barua ya kutaka mradi huo usitishwe kwa madai ya kukosa kuzingatia utaratibu ufaao.

Wakizungumza na wanahabari katika soko la Changara, wananchi hao wameelezea umuhimu wa mradi huo kwa jamii ikizingatiwa kuwa wenyeji wa eneo hili wamekuwa wakihangaika kutafuta maji.

Hata hivyo mwanakandarasi huyo Cleophas Mamai amesisitiza kuwa sharti matakwa yake yatimizwe ikiwemo kubuniwa kwa kamati ya kusimamaia mradi, matakwambayo wananchi wanasema yametimizwa huku wakimshutumu mwanaharakati huyo kwa kulemaza mendeleo katika eneo hilo.