Mwanaume taabani kwa kumwoa mwanafunzi aliyemhadaa kuwa wa miaka 18

teen pg
teen pg
Mwanaume wa umri wa miaka 25 alikana mashtaka ya ubakaji wa msichana mwenye umri wa miaka 15, Jumatatu.

Timothy Simiyu ambaye alishtakiwa kwa makosa ya kumbaka msichana mdogo, hata hivyo alikana mashtaka akisema kwamba alimhadaa kuwa alikuwa na umri wa miaka 18.

Simiyu alitekeleza kitendo hicho katika makaazi yake ya Lunga Lunga Nairobi, Juni 1. Alidaiwa kumwoa msichana huyo kwanzia Juni 1 hadi Novemba 10 ambapo alikumbwa na mkono wa sheria.

Kulingana na mashtaka dhidi yake, Simiyu alikutana na msichana huyo January na kumwagiza kwenda kwenye mkahawa moja lakini akakataa kwa kuwa alikuwa na kakake mdogo.

Hata hivyo, walikutana baadaye ambapo kidosho huyo alikubali kuwa mpenzi wake.

Simiyu alimkaribisha kwake na alipomwuliza umri wake, alisema ni 18 huku akiwa kwenye kidato cha tatu, alisema.

Aidha, alijitetea kwamba alimsihi arejee shuleni ila akadinda, huku akisema kwamba hakutaka Simiyu amwoe mwanamke mwingine.

Hapo ndipo waliishi pamoja kama mke na mume.

Majirani walimripoti kwa mzee wa kijiji kwa kukisia kwamba mkewe Simiyu hakuwa amefikisha umri wa miaka 18.

Simiyu alikana mashtaka hayo mbele ya hakimu mkuu Angelo Kithinji na akaachiliwa kwa dhamana ya shilingi 300,00 na mdhamini wa kiasi hicho.

Kesi hiyo itaskizwa tena Machi 16, mwaka uchao.