Mwanaume wa miaka 43 anapata nafuu katika hospitali ya isiolo baada ya kuvamiwa na Tembo

17076743_1491963654155205_5072012353990557696_n (1)
17076743_1491963654155205_5072012353990557696_n (1)
Mwanamume mwenye umri wa miaka 43 aliepuka kifo baada ya kushambuliwa na tembo watatu katika kijiji cha Ndunyuruma, sehemu ndogo ya Kithima kata ya Meru siku ya Jumapili.
Jotham Baariu alikuwa ananyunyizia maji vitunguu vyake akiwa na rafiki yake wakati tembo watatu walijitokeza kutoka kwenye msitu ulio karibu.
Alizungumza na vyombo vya habari katika Hospitali ya Isiolo ambako anapata nafuu. Alipata majeruhi kwa miguu na kifua.
"Tulikimbilia maisha yetu tulipoziona tembo na tulikimbia kwa njia tofauti, lakini tembo wale waliendelea kumfuata. Nilijificha katika kichaka, lakini tembo zilinizunguka. Moja ya tembo wale ilinichukua na kunivuta juu, umbali wa mita kumi, na kuniumiza kifua na miguu yangu." Alisema
Chifu wa Kithima, Paul Muriira alisema kwa miaka kadhaa, tembo wamekuwa wakiwasumbua wakazi wa Kithima, na maofisa wa KWS mara nyingi wanazifukuza kwenye hifadhi yao huko Isiolo.

 "Mara nyingi tembo hizo hurudi kwa sababu ya ukosefu wa malisho katika viwanja vya mbuga. Hata hivyo, hii ndio mara ya kwanza tembo hizo kushambilia mtu katika eneo hilo."alisema.
Msimamizi alitoa wito kwa Huduma ya Wanyamapori ya Kenya ili kuwalipa fidia wenyeji walioathirika. Alisema kuwa Jotham aliyejeruhiwa ndiye aliyekuwa anaitafutia familia yake chakula kwa hiyo familia hiyo itahitaji msaada wa haraka kwani hawezi tena kufanya kazi kwa muda hadi apate nafuu.
Soma mengi hapa