maji moto

Mwanaume Wa Miaka 76 Achomwa Na Maji Moto Na Mkewe Kufuatia Mzozo Wa Kinyumbani

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 76 kutoka kijiji cha Kapchemwam Kaunti ndogo ya Hamisi anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Vihiga mjini Mbale baada ya kuchomwa na maji moto na mkewe kufuatia mzozo wa kinyumbani

Kwa mujibu wa mhasiriwa ni kwamba aliweza kuvamiwa mnamo alhamisi iliyopita na mkewe wa miaka 66 nyakati za usiku baada ya mzozo wa kawaida wa kinyumbani, uliopelekea mkewe kujaribu kumnyonga tukio ambalo lilitibuka baada yake kujinasua kufuatia mvurutano wa muda.

Amehoji baada ya tukio hilo alijitosa kwenye malazi yake kabla ya kugutushwa usingizini na maji moto ambayo mkewe alikuwa anayaandaa pasipo yeye kujua.

Afisa mkuu wa matibabu katika hospitali hiyo Emmanuel Ayodi amesema mgonjwa huyo alijeruhiwa aslilimia 28 ya mwili wake japo kwa sasa yupo katika hali shwari akiendelea kupokea matibabu.

-Rehema Osanya

Photo Credits: Wonderopolis

Read More:

Comments

comments