wamalwa

Mwanawe aliyekuwa makamu wa Rais Kijana Wamalwa ameaga dunia!

Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa amesema kuwa uchunguzi utafanywa kwa mwili ya William Makali hapo kesho kubaini sababu cha kifo chake.

William Makali alikuwa mwanawe makamu wa Rais marehemu Kijana Wamalwa.

Waziri huyo alisema kuwa William aliaga dunia jumapili jioni baada ya kukimbizwa hospitalini kupata matibabu.

Eugene aliongeza kuwa William alikuwa buheri wa afya siku ya jumamosi na hata alishinda na marafiki wake, lakini siku ya jumapili alipatikana nyumbani kwake kama amepoteza fahamu.

Mwanamke akamatwa kwa madai ya kushiriki mapenzi na mvulana wa sekondari

 Waziri huyo alieleza kuwa mipango ya mazishi imeanza na William atazikwa jumamosi ijayo.

Vile vile alisema famila itatoa ripoti ya sababu cha kifo chake baada ya kutolewa kwa postmoterm.

William alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Nairobi.

Unachofaa kujua iwapo unapanga kuandamana kwa ajili ya kukamatwa kwa Sonko

 

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments