Mwanawe gavana Ferdinand Waititu afunga pingu za maisha (PICHA)

Mwanawe gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu, Monica Njeri alifunga pingu za maisha siku ya Jumamosi.

Shere ya harusi kati ya Monica na mumewe Daktari Nyotu Gitau ilifanyika katika kanisa la P.C.E.A Evergreen, Runda huku wakila chakula cha mchana eneo la Windsor Golf and Country Club.

Harusi hiyo ya kufana ambayo ilihudhuriwa na walioalikwa pekee, ilikuwa na jamaa na marafiki ambao walishuhudia sherehe hiyo. Ambao walihudhuria ni aliyekuwa mama wa taifa, Ngina Kenyatta, gavana wa Nyandarua Francis Kimemia na wengine wengi.

Kulingana na mtandao wake wa kijamii, daktari Nyotu alisomea Health Innovation katika chuo kikuu cha Cape Town na MBCHB, ana shahada ya udaktari na shahada ya upasuaji kutoka chuo kikuu cha Nairobi.

Njeri naye alisomea somo la udaktari katika chuo kikuu cha Nairobi.

Kwa sasa yeye ni daktari mkuu katika hospitali ya Gatundu Level 5 baada ya kuajiriwa na kaunti ya Kiambu.

Kabla ya hiyo alifanya kazi katika hospitali kuu ya Kenyatta.