Mwanawe Zari aweka bayana uhusiano kati ya mamake na Diamond

4OZOHa3i.jfif
4OZOHa3i.jfif
Mwanawe Zari Hassan, Raphael Ssemwanga amezungumzia kwa mara ya kwanza uhusiano wa kimapenzi kati ya mamake na mwanamuziki Diamond Platinumz

Rapheal alisema hangeingilia kati uhusiano wao kwani Diamond alikuwa akimpatia raha alohitaji mamake.

Akiulizwa iwapo alikuwa akiwasiliana na Diamond, Rapheal alisema haikuwa kila wakati kwa sababu alikuwa shuleni muda mwingi.

"Jambo hilo halikunitatiza kwa sababu Diamond alikuwa akimpatia mamangu raha wakati huo, singefanya lolote huyu ni mamangu na atabaki kuwa mama, sikuona tatizo yeye kupendwa na Diamond," Rapheal alisema.

Aidha, Rapheal alifichua kuwa sio rahisi azungumze na Diamond kwa sababu yeye hupiga simu kwa wakati mwingi akitaka tu kuzungumza na Tiffah na Nilan ambao ni watoto wake.

Rapheal pamoja na ndugu zake wanaishi Afrika Kusini na mama yao ambako pia wanasomea.