Mwandishi Mochama kulipwa fidia ya milioni 9, kwa kuharibiwa jina

Mwandishi Tony Mochama
Mwandishi Tony Mochama
Mahakama imemtunuku mwandishi Tony Mochama shilingi milioni tisa kama fidia katika kesi ya kumharibia jina.

“I find that the publication was malicious on a balance of probability and I am not satisfied that they established justification or fair comment. There was proof of injury to Mochama’s reputation. The award is fair and reasonable,” alisema

Habari zingine:

Hakimu alishikilia kwamba maneno hayo yalikuwa ya kumchafulia jina mtu na yalilenga kudhihaki na kudhalilisha hadhi ya Mochama kupitia mitandao ya kijamii. Alisema wawili hao wana elimu ya kutosha na wangefahamu kwamba maneno waliochapisha yalikuwa ya kupayuka na walikosea kutumia mitandao ya kijami kusambaza taarifa ya kumchafulia jina Mochama bila kuwepo kwa ushahidi wa kutosha.

“I have considered the legal position and re-looked the tweets as well as the threads on Mochama’s documents. The truth of these tweets concerning Mochama has not been established,” alisema.

Habari zaidi:

Mochama aliambia mahakama kwamba taarifa zilizichapishwa kwenye twitter zilikuwa na hila na za kumchafulia jina. Alisema kwamba kuchapishwa kwa taarifa hizo kulifanya aonekane mtekelezaji wa dhulma za kimapenzi na mnajisi.