Mwangi Kiunjuri amezindua chama chake cha kisiasa

EbRZ1npXkAEdgkv
EbRZ1npXkAEdgkv
Aliyekuwa waziri wa Kilimo nchini Mwangi Kiunjuri amezindua chama chake cha The Service Party [TSP] miezi sita tu baada ya kutimuliwa na rais Kenyatta kama waziri.

Kulingana na Kiunjuri, msajili wa vyama vya kisiasa nchini amewaruhusu kuendesha shughuli za usajili wa wanachama baada ya kuafikia viwango vinavyostahiki.

Amesema lengo la kuzindua chama hicho ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma mwafaka kutoka kwa viongozi.

'I’d like to introduce the entry of The Service Party of Kenya (TSP) into Kenya’s Politics… We have made the commitment to bring forth a platform that will be unequivocal about service delivery to our people as our name suggests',Kiunjuri