Aliyekuwa seneta wa Nyeri Mutahi Kagwe amerejea katika baraza la mawaziri kama waziri wa Afya Naye Betty Maina ndiye waziri mpya wa Viwanda . Rais Pia amewateua makatibu wapya wa kudumu katika wizara na makatibu wa utawala katika wizara mbali mbalimbali kama ifuatavyo-John Weru ameteuliwa kuwa katibu wa kudumu wa Wizara ya biashara ,Juan Ouma ni katibu wa kudumu wa mafunzo ya anuwai , Mary Kimonye ameteuliwa kuwa katibu wa kudumu wa Utumishi wa umma , balozi Simon Nabukhwesi ameteuliwa kuwa katibu wa kudumu wa elimu ya vyuo vikuu na utafiti , Solomon Kitungu ameteuliwa kuwa katibu wa kudumu wa Uchukuzi , Enock Momanyi Onyango ameteuliwa kuwa katibu wa kudumu wa Mipango ya Majengo , Joe Okudo amehamishwa kuwa katibu wa kudumu wa Michezo ,Chris Kiptoo sasa ndiye katibu wa kudumu wa Mazingira , Kevit Desai ndiye katibu wa kudumu wa jumuiya ya afrika mashariki ,Margaret Mwakima sasa ndiye katibu wa kudumu wa ustawi wa maeneo ,Esther Koimett ndiye katibu wa kudumu wa matangazo na mawasiliano,Peter Kaberia sasa ndiye katibu wa kudumu wa madini , safina kwekwe ndiye katibu wa kudumu wa Utalii na Collete Suda ndiye katibu wa kudumu wa Jinsia .
Rais Kenyatta pia amefanya uteuzi wa makatibu wa utawala katika wizara mbali kama ifuatavyo-
Hussein Dhado –CAS Wizara ya Usalama wa ndani
Patrick Ole Ntuntu- CAS Wizara ya Leba
Andrew Tuimur –CAS Wizara ya maji
Abdul Bahari –CAS Wizara Ugatuzi na maeneo ya ASAL
Lawrence Karanja – CAS wizara ya Viwanda na Biashara .
Peter Odoyo – CAS Wizara ya Ulinzi
Maureen Magoma Mbaka- CAS Wizara ya ICT na Ubunifu na masuala ya Vijana
Winnie Guchu – CAS Wizara ya Sheria ya Serikali
Wavinya Ndeti – CAS Wizara ya Uchukuzi
Zachariah Mugure –CAS Wizara ya Elimu
Mumina Bonaya – CAS Wizara ya Elimu
Lina Jebii Kilimo – CAS Wizara ya kilimo ,mifugo na Uvuvi
Ann Mukami Nyaga- CAS Wizara ya ya kilimo ,mifugo na Uvuvi
Mercy Mwangangi – CAS Wizara ya Afya
Nadia Ahmed Abdalla –CAS Wizara ya ICT ,Ubunifu na masuala ya vijana .