Mwarabu Fighter asimulia masaibu WCB. Asema Inama ya Diamond ina ukweli

Diamond_Platnumz_bodyguard_shows_off_accident_wounds-min
Diamond_Platnumz_bodyguard_shows_off_accident_wounds-min
Aliyekuwa mlinzi wa staa wa Bongo Diamond Platnumz sasa anadai kwamba ngoma ya Inama ya Mondi na Fally Ipupa inaeleza wazi yaliyojiri ili kupelekea yeye kutoka WCB.

Mwarabu anasema kuwa ukweli wanaujua ila hawataki kuusema.

“Diamond Platnumz anaujua ukweli lakini pia Harmonize anaujua ukweli, wao wanatumia nyimbo zao kufikisha ujumbe lakini hawataki kuongea ukweli.

"Mi nafurahi wanavyoniongelea kwani bado wanakumbuka makubwa niliyowafanyia”

Soma hadithi nyingine:

Mlinzi huyu aidha amezungumzia tofauti iliyopo katika maisha yake ya sasa na zamani alipokuwa mlinzi wa Mondi.

Katika wimbo wa Inama, Diamond anataja kwamba Harmonize alichangia pakubwa kufukuzwa kwa Mwarabu Usafini.

Katika mahojiano, Mwarabu amesema kuwa alihangaika sana kwa sababu hakuwa na hela.

"Nilipoacha kazi nilihangaika sana maana sikuwa na hata senti , mke wangu aliuza ngege mtaani ili tupate chochote..." Aliendelea kusimulia.

Mwarabu anasema kuwa vijana waige mfano wake,

Soma hadithi nyingine:

 "Vijana wengi wajifunze kupitia kwangu. Mimi niliishi kuilinda brand ya Diamond Platnumz. Mfukoni sina kitu..."

"Niliishi ili niendane na Brand ya msanii mkubwa lakini katika nafsi yangu niliumia sana..."

"Wakati huo sikuwa na gari wala pikipiki wala chombo chochote cha usafiri lakini nilikuwa napanda magari ya kulipia...”

Mistari ya wimbo huo unaonyesha dalili za kuwa Mwarabu alichepuka na Sarah wa Harmonize.