Mwenendo mpya katika tohara za wanawake (FGM)mkoa wa Mt Elgon

191777.131.3F987CD4(5)
191777.131.3F987CD4(5)
Tohara za wanawake zimekuwa tamaduni ya kitambo na zoezi la kitambo katika jamii ya Sabaot mkoa wa mlima Elgon. Licha ya ukweli kuwa zoezi la tohara ilipigwa marufuku, tohara wa kijadi waliweza kutoa mfumo mpya wa kufanya tohara.

Akiongea katika siku ya kitaifa ya (zero tolerance) dhidi ya FGM, Kopsiro ambaye ni naibu kaimu tume wa kata bwana David Bowen alibainisha kuwa zoezi hilo la tohara kwa wanawake lina fanywa na wakunga wa jadi.

Naibu wa mkuu wa kata aliweza kuwauliza wanawake wote ambao wanajifungua kuweza kutembelea vituo vya afya ambapo malipo yao yatashughulikiwa na kundi la wa mama (Linda mama programme).

Aliwaakikishia kuwa sheria ya utekelezaji wa wakala imekuwa ikifanya kazi kote ili kukomesha zoezi hilo kabisa.

Kemei pia alihusisha kupuguzwa kwa semina na mafunzo kufanyika katika waliokuwa jadi wa tohara kisha kufunzwa athari hasi za tohara kwa mwanamke FGM.

Kemei ambaye ni mwenye kundi liitwalo (Cheroto women group) alisema licha ya wao kukubali marekebisho au kubadilika, serikali haijaweza kukipa kikundi hicho pesa za kujikimu kimaisha.

"Wamawake wengi wanapitia changamoto hasa baada ya kurekebika, wanawake wengi hawana nyumba nzuri na wanaishi katika maisha ya umaskini huku ikiwalazimu kurudi katika zoezi la tohara ili waweze kupata kitu ya kujikimu," Alieleza Kemei.

Aliyekuwa mgeni rasmi katika afla hiyo ambaye ni (miss tourism) wa Bungoma Bi.Joyce Nasambu aliwauliza wakazi wa eneo la mlima Elgon waweze kuacha zoezi hilo na kusema kuwa ataendelea na kampeni na kutimiza kukomesha tohara ya mwanamke FGM.

Nasambu aliweza kuwapongeza wanawake ambao walibadilika na kisha wakapeana visu ambavyo walikuwa wanatumia katika zoezi la tohara kisha akawapa zawadi za kuwapongeza kwa ujasiri wao.

Joyce ambaye amejitoa kumaliza zoezi la tohara ya mwanamke FGM aliweza kuwauliza wanawake walio badilika kusaidiana na kungoja fedha za kikundi hicho bila wasiwasi.

"Nitaleta tahadhari ya kubadilika kwenu kwa gavana kisha aweze kuwaunga mkono na kuleta watu wenye mapenzi mema kwenye bodi ili waweze kuwasaidia na pesa na si pesa tu kuwasaidia kwa mambo mengi katika kikundi hiki," Alibaini Kemei.

Kai pia aliweza kusema kuwa wataweza kuleta miradi tofauti kwa wanawake hao ili ambayo itaweza kukomesha tohara kwa wanawake  na pia miradi ambayo itawasaidia kujikimu kumaisha.

Alisema pia mipango iko katika mawazo yao ya kuanzisha biashara tofauti na pia kujifunza kilimo ili wasiwe na shida yeyote, pia aliweza kuwauliza wadau wawaunge mkono wanawake hao.

"Tunawaomba wadau waweze kuwasaidia na kuwaunga mkono wanawake hawa pia kuhakikisha kuwa wanaishi maisha mazuri na meme," Alisema Kakai.

Aliweza tena kuwahidi kuwa ataweza kuanzisha masomo kwa wanawake ili kukomesha tohara za mwanamke eneo la mlima Elgon.