Mwili wa Bob kuchomwa Kariakor ! Orodha ya viongozi waliochomwa baada ya kuaga

Familia nyingi nchini zinaukumbatia zaidi mtindo wa kuchoma miili ya wafu kama njia moja ya kuwapa heshima zao za mwisho. Kuchoma mwili kwa kawaida ni zoezi ambalo huwa linachukua kama masaa mawili na nusu.

Soma hapa hadithi nyingine:

Kuchomwa kwa mwili wa mtu mzima ni kati ya shilingi 9,ooo - 13,000. Bei ya kuuchoma mwili wa mtoto ni takriban shilingi 4,000-6,000.

Tunakusogezea hapa orodha ya viongozi waliowahi kuchomwa baada ya kufariki:

1. Wangari Mathai

Wangari alifariki mwaka wa 2011 na mwili wake kuchomwa tarehe 8 Oktoba, 2011 Kariokor.

2. Kenneth Matiba

Kenneth Matiba alikuwa mwanasiasa nchini. Alikuwa katika mstari wa kwanza kupigania demokrasia. Alifariki Aprili 15 ,2018 na mwili wake kuchomwa tarehe 27 Aprili , 2018 Lang'ata.

Soma hapa hadithi nyingine:

3. John Macharia

John alikuwa mtoto wake SK Macharia. Alifariki mwaka wa 2018 katika hospitali ya Karen. Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, mwili wa mwanawe Macharia ulichomwa katika makaburi ya Lang'ata.

4. Jeremiah Kiereini

Jeremiah Kiereini alifariki akiwa na umri wa miaka 90 .

5. Githae Kiereini

Alikuwa mwanawe marehemu Jeremiah Kiereini. Mwili wake ulichomwa mwaka wa 2017 baada ya kupatikana amefariki katika gari lake.