Mwili wa mwanaharakati wa Dandora aliyepotea kupatikana

Ni kitendawili kwa wananchi wa Dandora na familia ya mwanaharakati Caroline Mwatha aliyepotea wiki iliyopita kisha kupatikana katika chumba cha kuhifadhi maiti.

Wananchi wameingiwa na hofu kwa maana mwananchi yeyote akipotea harudi nyumbani akiwa hai bali anarudi akiwa amefariki, na kisha maswali kujawa katika akili za familia.

Lakini ni nani hao hawana roho za utu ili kuwauwa wanadamu kama wanyama wasiokuwa na hatia?

Caroline aliripotiwa kupotea jumamosi wiki jana, huku polisi wakifanya wawezalo ili kumtafuta mwanaharakati huyo, hawakuchoka mtafuta Caroline bali walitia bidii ya mchwa hadi kumtafuta hadi kwenye misitu na maji.

Polisi waliweza kusema kuwa mwili wa Mwatha ulipelekwa katika chumba hicho siku baada ya kupotea kwake, ilhali familia walisema kuwa baada ya kuarifiwa kupotea kwake waliweza kuenda kumtafuta kila hospitali na nyumba za kuifadhi maiti na hawakuweza kumpata.

Lakini kwanini apelekwe katika chumba cha maiti siku baada ya kupotea na kisha kuenda kutafutwa na familia na kuambiwa hakuna mtu aliye na jina kama hilo maeneo hayo?

Kitambo Jumanne familia iliweza kupigiwa simu na kuambiwa kuwa mwili wa Mwatha umepatikana katika mto na kuenda kuuona.

Polisi aliyetaka kutojulikana alisema kuwa walipigia familia ya Mwatha tena na kuwajulisha kuwa mabaki ya mwili si ya msichana wao Caroline.

Maafisa walisema kuwa waliweza kujibu baada ya wanachama wa taifa kupiga simu katika kituo cha polisi na kusema kuwa wameona mwili kando ya barabara.

"Hata hivyo hatuchukui nafasi yeyote, tuta zidisha au kupanua kutafuta ukweli katika kila mahali risasi itakuwa tutumie," Alisema polisi.

Mwatha alikuwa afisa mkuu katika kundi la Dandora Community Social justice Center. Alikuwa anahusika na kesi ya mauaji yasio na hatia na kisha kesi ya mauaji ya damu baridi ya watu sita waliopigwa risasi na polisi Oktoba mwaka jana.

Katika kauli ya mkurugenzi mtendaji wa Amnesty International aliweza kuwaomba maagendi wa uchunguzi kumtafuta Caroline na kuwajulisha mahali alipo.

Si kesi ya kwanza ya mwananchi kupotea na kurudi kwake akiwa maiti, ni watoto wamebaki yatima na mume wa Caroline kubaki mjane wasijue kisicho sababisha kifo cha mwanaharakati huyo.