Mwili wa mwanamke asiyejulikana wapatikana mto Sio, Busia

Mwili wa mwanamke ambaye hajulikani umepatikana ukielea kwenye mto sio katika kijiji cha nasewa eneo la Matayos kaunti ya Busia.

Mwili huo ambao ulikuwa uchi ulikuwa na majeraha ya panga kichwani, kunyongwa shingoni na kuchomwa na kifaa cha plastiki mikononi na miguuni, uligunduliwa na wakaazi wawili wa kijiji hicho ambao walikuwa wameenda kwenye mto huo kuvua samaki.

Chifu wa eneo hilo Stephen Wawire ameungana na wenyeji wa eneo hilo kuwarai wale ambao jamaa wao ametoweka kwenda kwenye chumba cha wafu cha hospitali ya rufaa ya busia ili kuutambua mwili huo.

Hayo yakijiri, mzozo kati ya wafugaji wa kuhamahama na wenye mashamba ya malisho katika kaunti ya Taita Taveta umetajwa kuchangiwa na mikataba ambayo si halali.

Jopo lililoundwa kuchunguza uhalali wa mikataba kati ya wafugaji na wamiliki wa mashamba ya malisho katika kaunti ya Taita Taveta limefichua kuwa sheria haikufatwa katika kuandikishana mikataba hiyo.

Naibu mwenyekiti wa jopo hilo ambaye pia ni waziri wa mazingira, ardhi na mali asli Mwandawiro Mghanga anasema kuwa jopo hilo limependekeza kuvunjiliwa mbali kwa mikataba hiyo na uundaji wa sera bora za kudhibiti uingizaji wa mifugo katika kaunti hiyo kiholela.

-Leonard Acharry/Solomon Muingi