Mwili Wa Mwanaume Mwenye Umri Wa Makamu Wapatikana Migori

mwili
mwili
Polisi huko Kuria magharibi kwenye kaunti ya Migori wameanzisha uchunguzi baada ya mwili wa mtu mmoja kupatikana ameuawa katika kijiji cha Getonganya kwenye kaunti hiyo.

Kulingana na OCPD wa Kuria magharibi Evans Wanyonyi mwili wa marehemu Marwa Kerato wa umri wa miaka arobaini na miwili ulipatikana umekatwa kichwani na kifaa butu baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo.

Wanyonyi alisema kuwa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho baada ya watu hao kuvamia mtu huyo bila ya kuiba chochote katika nyumba yake na pia hawakujeruhi mtu mwingine ila tu mwenye boma.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya kibinafsi ya Pastor Machage mjini Migori ukisubiri kufanyiwa upasuaji.