Mwimbaji Mashuhuri Wahu Akana Tetesi za Ujauzito

Tangia mwanzo wa mwaka huu, mwimbaji wa nyimbo za injili Wahu, amedhaniwa kuwa mjamzito. Tangu tetesi hizo zienee, angetarajiwa kwa sasa kuwa mjamzito sana na tumbo la uzazi kuonekana, lakini hali si hiyo!

Nameless, mwimbaji mashuhuri na mume wa Wahu, alisita kuongelea swala hilo alipoulizwa ikiwa wanatarijia mgeni mwingine katika familia yao.

Alisema:

            ”Hahahaaa. Sina la kusema.”

Wahu alithibitishia umati kuwa walivyo dhania sivyo. Siku ya Jumamosi alihudhuria tamasha ya kutuzwa, akiwa amevaa nguo nyeupe, huku akiongozana na mume wake.

Tuseme tu uvumi huo ulisambazwa kwanza na mashabiki ambao walihisi kuwa Wahu alikuwa anawapa dhana ya kuwa ana ujauzito kwa kuposti picha nusu kwenye mitandao ya kijamii.

Meneja wa Sauti Sol, Marek Fuchs, ana nyumba ya kutamanika (picha)

 

wahu

Kutokana na picha hizi ni wazi kuwa hategemei kujifungua mtoto mwingine wakati wowote hivi karibuni. Wahu ni mama ya watoto wawili wa kike wanaoonekana kukua haraka sana.

 

Nyakati za mwisho za E-Sir, Nameless afichua jini la E-Sir la mfuata

Tangu aweke wazi kwa mashabiki wake kuwa ameokoka na kumwacha Mungu ashike uskani maishani mwake, anaonekana kushikilia mwito huo na anaendelea kufanya ushirikiano na wanamziki wengine wa nyimbo za injili kutoa nyimbo za kumsifu Mungu.

Wahu azidi kuwashauri mashabiki wake kuwa kile ambacho binadamu anadhani si muhimu kama ambacho Mungu anafikiria.

Photo Credits: Facebook

Read More:

Comments

comments