Mwisho wa Ngono! Watafiti wadai huenda viruis vya Corona vikasalia katika mbegu za mwanamume

NA NICKSON TOSI

Virusi vya corona sasa vina uwezo wa kusalia ndani ya mbegu za mwanamume yaani semen's hata baaada ya kupona. Utafiti ambao unasema kuwa huenda sasa virusi hivyo vikaweza kusambazwa wakati wapenzi wawili wanaposhiriki ngono. Ni utafiti ambao umefanyiwa na mtafiti mmoja kutoka Uchina na kutoa ripoti hiyo Alhamisi.

Kikundi cha madaktari katika hospitali ya  Shangqiu Municipal Hospital iliwafanyia wanaume  38 waliokuwa wameathirika na gonjwa hilo hatari kati ya Januari na Februari na kubaini kuwa mbegu zao zilikuwa na chembechembe za virusi hivyo.

Asilimia 16 ya wanaume hao walionyesha chembechembe za corona kwenye mbegu zao ripoti ambayo wameichapisha kwenye nakala ya JAMAL Network Open.

“We found that SARS-CoV-2 can be present in the semen of patients with COVID-19, and SARS-CoV-2 may still be detected in the semen of recovering patients,” amesema daktari Diangeng Li

Daktari Li amesema kuwa hata kama virusi hivyo havitakuwa na uwezo wa kuzaana, huenda vikaathiri viungo vingine vya mwanamume na hata wakati mmoja kuufanya mwili wake kukosa uwezo wa kukabiliana na virusi hivyo.

“Even if the virus cannot replicate in the male reproductive system, it may persist, possibly resulting from the privileged immunity of testes,”aliongeza Li

Watafiti hao kwa ushirikiano na madaktari hawajabaini iwapo virusi hivyo pia vinaweza kusambaa kupitia njia ya ngono .