Kutoka taswira ya kipekee jua linapotua ,mbuga kadhaa za wanyama na mvuto wa maporomoko ya maji.kutoka milima ,na maziwa ya kuvutia ,fuo za bahari ,visiwa miongoni mwa vingine ,kenya ni jungu la kila unachoweza kutaka kutazama .
Tuangalie baadhi ya sehemu ambazo unafaa kuzuru nchini kenya .
Pwani
Pwani ,ina historia ya kipekee na asili na ni ngome ya wa mijikenda na waswahili .
Sehemu hii ndio tisha ya kuburudika na kupumzika .mvuto wake hauna ubishi !utaweza kuwashuhudia ngamia wakitembea pembeni mwa ufuo wa bahari .maji yenye rangi ya samawati kwa mbali pia yanakupa picha itakayodumu fikrani kwa muda .
Watalii wengi kutoka sehemu mbali mbali za dunia huzuru eneo hili.
Maasai Mara
Mbuga ya kitaifa Maasai mara, ina wanyama wengi wa porini unaoweza kuwatazama na kujifurahisha .
utapata fursa ya kutangamana na hali halisi asili ya abara la afrika . utashuhudia ujasiri wa jamii zinazopakana na mbuga hii kama vile masaai ambao wamelelewa karibu na wanyama wa porini . Kuna Soga kwamba lazima wapigane na simba ili wawe 'wanaume'
Lake Naivasha
Ni mto wa maji yasio na chumvi nchini kenya na una maeneo bora sana ya kuweza kutawama wanya wa pori . utaweza kuwaona ndege wa flamingo wakiwa katika makaazi yao asili . unaweza kuwakaribia na kutangamana na wanyama kama vile chui , kifaru .
Mount Kenya
ni watu wachache duniani wameukwea mlima huu na wale waliofanya hivyo watakuambia una mandhari mazuri sana ya kuvutia . itakulazimu ujionee mwenyewe ili uweze kunufaika na mazuri yote katika Mlima huu .
Giraffe Centre
The Giraffe Center kipo mtaani Lang'ata kilomita 20 kutoka katikati wa jiji la Nairobi . kituo hiku kilianzishwa ili kuwalinda twiga ambao maisha yao yalikuwa hatarini afrika mashariki .
utaruhusiwa kuwa;lisga twiga hawa .Ni warefu sana utaweza kuwalisha ukiwa ndani ya hoteli ,unapoteremsha kiamsha kinywa .
Nairobi National Museum
Makavazi haya yanalenga kulinda utamaduni na turathi za kenya kando na kuwapa wageni fursa ya kufahamu historia na urithi wetu . kando na hayo wageni pia wana fursa ya kununua vitu na vyakula vya kipekee pamoja na kuzuru bustani zenye mimea inayokupa mandhari ya kipekee
Lamu Island
KISIWA cha Lamu kipo katika pwani ya kenya . kisiwa hiki kinafikiwa kwa usafiri wa boti hadi Mokowe na pia hadi kisiwa cha Manda ,ambapo kuna uwanja mdogo wa ndege . kina mvuto usioridhisha na hasa kwa wageni .