Mzee, 78, apatikana amefariki huku dawa za kusisimua uume zikipatikana

Mwili wa miaka 78 ambaye ni mwalimu mstaafu umepatikana kitandani katika mojawapo ya lodging zilizo katika mji wa Nyamira, kaunti ya Nyamira, siku ya jumanne.

Kulingana na chifu wa eneo hilo, Johnson Manyara, marehemu kwa jina, Saul Mokua, ambaye anatoka katika mtaa wa Bosamaro Chache, alionekana mwisho jumatatu na mwanamke wa umri wa makamu wakiingia katika klabu ya club 78 ilioko katika soko la Nyabite.

Manyara anasema baada ya kukagua lile jumba walipata pakiti ya tembe sita za dawa za kusisimua uume kando ya mwili wa mwendazake.

“WE FOUND WHAT LOOKED LIKE SEX ENHANCING PILLS BESIDES THE BODY AND IT IS SUSPECTED THE DECEASED MIGHT HAVE TAKEN AN OVERDOSE,” ALISEMA CHIFU WA ENEO HILO.

Hata hivyo, Manyara alisema marehemu mwalimu huyo mstaafu alikuwa na historia ya kuwa na shida ya shiniko la damu kulingana na jamaa zake.

Wakati huo huo, klabu hiyo ya club 78 bado haijafungwa kama ilivyo ahidiwa na kamshina wa kaunti ya Nyamira bwana Amos Mariba, mwishoni mwa mwaka uliopita, baada ya msichana wa shule kupatikana ndani mwa majumba hayo pamoja na jamaa wa bodaboda.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Kinara, Nyamira ukingoja kufanyiwa upasuaji.