Mzee taabani kwa kukosa kubadilisha noti mzee za elfu moja

Noti 1
Noti 1
Anasema kwamba pesa hizo zilikuwa ni pensheni yake ya uzeeni alikuwa amezificha mvunguni mwa kitanda baada ya kustaafu kutoka kampuni moja nchini.

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 60 kutoka maeneo ya Siaya anaomba Benki Kuu ikubali kumbadilishia noti za elfu moja ya zamani yenye thamani ya nusu milioni.

Julius Odinga Mboga ansema kwamba pesa hizo ambazo ni za uzeeni alizichukua benkini miezi michache tu baada ya kupokea.

Mzee huyo kutoka kijiji cha Sirondha anaishi kwa mshtuko mkubwa sasa baada ya kuambiwa kuwa noti zamani za elfu moja ambazo ni pensheni yake yenye thamani ya milioni 0.5 haina maana tena.

Kwa kile ambacho hakikufahamika wazi, mhandisi huyo wa zamani kutoka kampuni moja ya kibinfasi kule Limuru alisahau kuregesha pesa hizo hata baada ya kusoma notisi kutoka vyombo vya habari kuhusu makataa ya kuzirudisha noti hizo nzee za elfu moja.

Kulingana na hati zake, alizitoa pesa hizo benkini kima cha shilingi 200,000 Juni na shilingi 300,000 Julai mwaka huu.

"Aligundua kwamba noti ya elfu moja ya zamani haitumiki tena wakati alipolipia bili zake katika mkahawa moja.

Mzee Odinga si yeye pekee anayemiliki noti hizi nzee baada ya makataa ya tarehe 30 Septemba ambayo ilikuwa ni muda rasmi wa kuregesha pesa hizo kwa benki kuu.