Mzee Wa Miaka 65, Anusurika Kifo Baada Ya Kufumaniwa Akimbaka Mwanafunzi

ubakaji
ubakaji
Polisi mjini Bungoma wanamzuilia mshukiwa mmoja wa ubakaji kutoka kijiji cha Mteremko eneo bunge la kanduyi baada ya mshukiwa kufumaniwa na wakaazi chumbani mwake.

Joseph Wanakawa mwenye umri wa miaka 65 ambaye pia ni mmoja wa wazee wa kijiji hicho na kakake chifu wa eneo hilo anadaiwa kumnyemelea mwananfunzi wa darasa la tatu aliye na umri wa miaka minane alipokua akienda dukani kununua mandazi na kumbaka.

Maafisa wa polisi wa Bungoma waliofika mara moja eneo hilo walilazimika kutumia vitoa machozi kutawanya umati wa watu uliokuwa na ghadhabu ukitaka kumuangamiza mshukiwa aliyekua amejihami kwa kisu akitishia kumvamia yeyote aliyemzomea.

Watu wanne walijeruhiwa katika kisa hicho huku polisi wakianzisha uchunguzi wa kina kuhusu kisa hicho.