crime-scene-300x225

Mzee wa miaka 67, adaiwa kumbaka mtoto wa miaka kumi na miwili

Familia moja kutoka kijiji cha Shamala wadi ya Butsotso Mashariki eneo bunge la Lurambi inataka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mzee wa miaka 67 anayedaiwa kumnajisi mwanao wa miaka 12.

Jinsi kesi ya ubakaji ilimuumiza moyo Cristiano Ronaldo

Inasemekana Mzee huyo alimhadaa mwathiriwa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu kwa peremende kabla ya kumbaka.

Wakiongozwa na mamake Violet Busieka, walisema mzee huyo alifumaniwa mnamo Jumapili mchana kichakani na babake mtoto huyo kabla ya kutoroka na kumwacha alipokuwa akimfanyia kitendo hicho cha unyama.

Aidha wanadai kuwa hicho si kitendo cha kwanza kwa babu huyo kwani amewahibaka mtoto mwingine hapo awali.

Wakazi wanatishia kuchukua sheria mikononi mwao iwapo idara husika hazitatekeleza wajibu wao ipasavyo.

Chifu wa eneo hilo Emmmuel Shikanda anasema amepokea habari hiyo na wako katika harakati ya kumtafuta na kumtia mbaroni mshukiwa ili ashitakiwe.

Wachezaji waliopatikana na hatia ya ubakaji kuzuiliwa kwa wiki moja zaidi

-Sammy Mwibanda

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments